Lyrics

Ni nani huyo, Nimuonaye, Mtu wa nne, Ndani ya moto (Ni nani eeh) Ni nani huyo, Nimuonaye, Mtu wa nne, Ndani ya moto, Twamsoma Shadraki, Meshaki, Abedineko, Walipotupwa kwenye tanuru, Ili wateketee, Muujiza ukatokea, Yesu kaingia humo, Akawaficha na moto, Haukuwaunguza, (Ni nani eeh) Ni nani huyo, Nimuonaye, Mtu wa nne, Ndani ya moto Ni nani huyo, Nimuonaye, Mtu wa nne, Ndani ya moto, Na Nebukadineza, kashangaa, Kawaita mawaziri, kauliza, Je hatukuwatupa, watu watatu, Mbona sasa ninaona, wako wanne (Ni nani eeh) Ni nani huyo, Nimuonaye, Mtu wa nne, Ndani ya moto Ni nani huyo, Nimuonaye, Mtu wa nne, Ndani ya moto, Haleluya!! Naye ni nani atakaye washitaki, Wateule wa Mungu Jehova, Tena ni nani atakaye wahukumu, Wateule wa Mungu Jehova, Bali Mungu mwenyewe huwalinda, Tena Mungu mweyewe huwatetea, Bali Mungu mwenyewe huwalinda, Tena Mungu mweyewe huwatetea (Ni nani eeh) Ni nani huyo, Nimuonaye, Mtu wa nne, Ndani ya moto Ni nani huyo, Nimuonaye, Mtu wa nne, Ndani ya moto, Itakuwa kwako, mtu wa Mungu, Ukijaribiwa na mwovu, Yesu atakuja, vumilia, Kwenye shida yako, kukuponya, Itakuwa kwako, mtu wa Mungu, Ukijaribiwa, na mwovu Yesu atakuja, usihofu, Kwenye shida yako, kukuponya, Watashangaa, waliokushitaki, Wataulizana, imekuwaje, Watashangaa, walokutegea, Wataulizana, nani kamuokoa, Watashangaa, waliokushitaki, Wataulizana, imekuaje, Watashangaa, waliokutegea, Wataulizana nani, kamuokoa, Nawe utasema, ni Yesu, Halleluyah!!! Tena utasema, ni Yesu, eeh Ni Yesu, amenitendea, (Aah ni Yesu eeh) Ni Yesu amenitendea, (Yeye Bwana ananipenda sana, halleluyah) Ni Yesu amenitendea, (Yeye Bwana ananijali mimi, halleluyah) Ni Yesu amenitendea, (Yeye ndiye mlinzi wangu Bwana, halleluyah) Ni Yesu amenitendea (Yeye ndiye mtetezi wangu Bwana, halleluyah) Ni Yesu amenitendea... (Nataka niseme na wewe uliye kata tamaa Inawezekana umetupwa Kwenye tanuru la moto Naomba uvutie moyo Yesu ambaye ni mtu wa nne Yuko pamoja nawe na atakwenda kukuinia tena halleluyah) Amen (Wewe mjane uliye nyimwa haki yako Usiogope maana Mungu aliye Mme wa wajane yuko pamoja nawe Na atakurejeshea yale yote uliyopoteza sema amen) Amen (Wewe yatima Mungu anakupenda Hata kama unajiona uko pekee yako Lakini Mungu aliye Baba wa yatima yuko pamoja nawe Usiogope maana atakutunza halleluyah Uko muujiza kwa ajili yako Wewe usiye na kazi Uko muujiza kwa ajili yako Wewe mama usiye na mtoto Nasema uko muujiza wa uponyaji wa magonjwa yako Uko muujiza kwa ajili ya masomo yako Ndugu yangu uko muujiza kwa ajili yako Maana yeye Yesu alichukia mateso yetu na taabu zetu Pale msalabani na huzuni yako ameniona Machozi yako ameyaona usiogope Kama alivyowatetea Shadraki, Meshaki na Abedneko Hata kwaja kwako leo sema Amen) Amen (Sema Amen) Amen (Hebu twaweza tukaimba pamoja Ni Yesu amenitendea Hata kama unaona giza lakini Mungu anatenda kitu kwa ajili yako) (Ni yesu amenitendea aah ni Yesu eeh) Ni yesu amenitendea (Yesu anapigana na adui zako sasa, -- halleluyah) Ni yesu amenitendea (Usiogope maana yeye yuko pamoja nawe, halleluyah) Ni yesu amenitendea (Atakuuisha na kuku Ni yesu amenitendea (Ndiyo maana ninampenda Bwana, halleluyah) Ni yesu amenitendea (Ndiyo maana ninamwimbia yeye, halleluyah) Ni yesu amenitendea (Ndiyo maana ninamsifu Bwana, halleluyah) Ni yesu amenitendea (Ooh ni Yesu eeh, halleluyah) Ni yesu amenitendea (Aah a ni Yesu eeh, halleluyah aaaah) Ni yesu amenitendea
Writer(s): Kinondoni Revival Choir Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out