Music Video

ZABRON SINGERS - NIFUNDISHE (official video)
Watch ZABRON SINGERS - NIFUNDISHE (official video) on YouTube

Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Zabron Singers
Zabron Singers
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Marco Joseph Bukulu
Marco Joseph Bukulu
Songwriter
Emmanuel Zabron Philipo
Emmanuel Zabron Philipo
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Marco Joseph Bukulu
Marco Joseph Bukulu
Producer

Lyrics

[Intro]
Anatupenda
Hii hii hii
Anatupenda
Anatupenda
Hii hii hii hii hii
Hii hii hii hii hii
[Verse 1]
Maisha ya mwanadamu kuishi kwake huwa mara moja
Yakishapita yakishapita huwezi kuyarudisha
Mbona twaishi twaishi kwa nguvu za Mungu pia uwezo wake
Tumkumbuke Mungu siku za uhai wetu
Kama unataka muijiza ni huu hapa sasa
Wa wewe kuamka
[Verse 2]
Hee je ni wangapi wamelala wakashindwa kuamka kwani we ni nani au
Unafikiri uzuri wako umekufanya uwe hai au ni dakitari wako?
Heii si kwa nguvu zangu mimi wala nguvu zako wewe ni kwa nguvu zake Mungu mmh
Ndio maana tuko hai anazidi kutulinda ameonekana kwetu uu
[Chorus]
Nifundishe
Nifundishe kukutegemea kwa hali zote ninazopitia
Hata kwa magumu yote kwa magumu Baba, ngome yangu
Wewe ndio kimbilio langu na ngome yangu haleluyaa
Nifundishe Baba (Fundishe Yesu, hali zangu)
Hata kwa magumu yote kwa magumu yangu, Baba yangu
Wewe ndio kimbilio langu na ngome yangu haleluyaa
[Bridge]
Wanijua Baba
Hee wanijua Baba wanijua Mungu
Hali yangu
[Verse 3]
Alisema giza liwe nalo likawa haah
Kwa fimbo Musa bahari akaigawa haah
Tanuruni aliwaacha midomo wazi
Heheeh mtu wa nne katoka wapi?
[Verse 4]
Kwa kugusa pindo yule mama kapona haah
Batimayo nae kapona kwa mate na tope
Hajaanza jana na wala haishii leo
Ni Mungu wa yakobo Daudi Milele amina
[Verse 5]
Hebu fikiria Imani yako ilivo ndogo
Na matendo yako bado anakulinda badoo
Ni dhahiri kuwa Mungu wetu huyu
Anatupenda, anatupenda, anatupenda
Haleluyaa
Anakupenda kupenda ulivyo, ulivyo wewe Mungu wangu
Anatupenda, anatupenda, anatupenda
[Chorus]
Nifundishe
Nifundishe kukutegemea kwa hali zote ninazopitia
Hata kwa magumu yote kwa magumu Baba, ngome yangu
Wewe ndio kimbilio langu na ngome yangu haleluyaa
Nifundishe Baba (Fundishe Yesu, hali zangu)
Nifundishe kukutegemea kwa hali zote ninazopitia
Hata kwa magumu yote kwa magumu yangu, Baba yangu
Wewe ndio kimbilio langu na ngome yangu haleluyaa
[Outro]
Anatupenda, anatupenda, anatupenda
Heey anakupenda ulivyo, ulivyo wewe Mungu wangu
Anatupenda, anatupenda, anatupenda
Ikiwa shwari mi nitaimba
Haleluya (Haleluya) haleluya aa
Hata kwenye dhiki mi nitaimba
Haleluya (Haleluya) haleluya aa
Ikiwa shwari mi nitaimba haah
Usifiwe (Usifiwe) usifiwee ee
Written by: Emmanuel Zabron Philipo, Marco Joseph Bukulu
instagramSharePathic_arrow_out