Music Video

jubilee by zabron singers (Official lyrics)
Watch jubilee by zabron singers (Official lyrics) on YouTube

Featured In

Credits

PERFORMING ARTISTS
Zabron Singers
Zabron Singers
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Marco Joseph Bukulu
Marco Joseph Bukulu
Songwriter
Emmanuel Zabron Philipo
Emmanuel Zabron Philipo
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Marco Joseph Bukulu
Marco Joseph Bukulu
Producer

Lyrics

[Verse 1]
Sikukuu ya vibanda imefika
Tumekuja kukutana wewe Mungu wetu
Tupokee mioyo yetu tumefika
Tutazitoa mali zetu na mioyo yetu
[Verse 2]
Familia zirekebishwe
Na ndoa zirekebishwe
Kwenye kutoa turekebishe
Imani iwe imara
[Verse 3]
Masengenyo tuache hapa
Wivu tuutawale
Uzinzi tuukemee
Na upendo ukatawale
[Chorus]
Biashara zetu tumeziacha
Tumekuja kukutana wewe Mungu wetu
Mashamba yetu tumeyaacha
Tumekuja kukutana wewe Mungu wetu
[Verse 4]
Ni desturi yako tukaenzi uzao wako ukae pamoja
Wakuabudu na kukusifu Bwana
Wafue mavazi wajitakase wafue mavazi ya mioyo yao
Iwe upatanisho wetu na wewe
[Verse 5]
Mbaraka kwa watu wote finyanga mioyo yao
Bariki watoto wako wakirudi wakutukuze
Na pale walipotoa rudisha wajaze tele
Na hivyo walivyonavyo viongezeke ukavitunze
[Verse 6]
Baba tuko kwako mbeba mambo yetu
Beba shida zetu kwenye hii jubilee, jubilee
Takasa mioyo yetu jinsi upendavyo
Tusitoke vile vile Baba tutakase mibaraka tubebe
[Refrain]
Hii ni jubilee bado tuko kwenye jubilee
Tubariki kwenye hii jubilee
Mibaraka iko jubilee
[Chorus]
Biashara zetu tumeziacha
Tumekuja kukutana wewe Mungu wetu
Mashamba yetu tumeyaacha
Tumekuja kukutana wewe Mungu wetu
[Refrain]
Eee na nyumba zetu tumeziacha
Tumekuja kukutana wewe Mungu wetu
Watoto wetu Bwana tumewaleta
Tumekuja kukutana wewe Mungu wetu
[Chorus]
Washiriki wote ona tuko hapa
Tumekuja kukutana wewe Mungu wetu
Wachungaji wetu ona wako hapa
Tumekuja kukutana wewe Mungu wetu
[Outro]
Hii ni jubilee bado tuko kwenye jubilee
Tubariki kwenye hii jubilee
Mibaraka iko jubilee
Written by: Emmanuel Zabron Philipo, Marco Joseph Bukulu
instagramSharePathic_arrow_out